Home Blog Article
Clearing & Forwarding 7 min read

Tofauti Kati ya Freight Forwarding na Clearing

M
melek
GNM Cargo Editor
Nov 10, 2025 78 views 1 comments

Wafanyabiashara wengi wanaanza safari ya uagizaji bila kuelewa vizuri tofauti kati ya freight forwarding na clearing, jambo linalosababisha mkanganyiko na wakati mwingine kupoteza muda au fedha. Kwa GNM Trading, tunahakikisha wateja wetu wanaelewa hatua zote ΓÇö kuanzia kupanga safari ya mzigo hadi kuupitisha kwa forodha ΓÇö ili wasiwe tegemezi kwa maelezo ya upande mmoja.

GNM Inatoa Huduma Zote Mbili

Tofauti na kampuni nyingi ambazo hufanya ama forwarding pekee au clearing pekee, GNM Trading inatoa huduma zote mbili kwa pamoja.
Hii ina faida kubwa kwa wateja:

Mteja anapunguza gharama kwa kuwa hakuna dalali kati ya forwarding na clearing.

Ufuatiliaji ni rahisi timu moja inasimamia safari yote ya mzigo kuanzia China hadi Tanzania.

Uwiano wa taarifa unakuwa sahihi, kwani nyaraka za forwarding zinatumika moja kwa moja kwenye clearing bila makosa.

Kwa kutumia mfumo wa kidigitali wa GNM, mteja anaweza kufuatilia safari ya mzigo wake kutoka supplier hadi dukani, kwa real-time updates na taarifa kamili za kila hatua.

Hitimisho

Kwa kifupi, freight forwarding ni kupanga safari ya mzigo wako, wakati clearing ni kupitisha mzigo wako kwa forodha ili uingie sokoni kisheria.
GNM Trading inakupa vyote mpangilio wa safari, usimamizi wa mizigo, ufuatiliaji wa kielektroniki, na clearance halali, yote chini ya paa moja, kwa ufanisi na uadilifu.

Forwarding Ni Kupanga Safari ya Mzigo

Freight Forwarding ni hatua ya kupanga safari ya mzigo kutoka kwa muuzaji (exporter) hadi kwenye bandari au mpaka wa nchi lengwa.
Hapa, kazi kuu ni kuhakikisha mzigo unafika salama, kwa wakati, na kwa gharama nafuu.
GNM Trading, kama freight forwarder, inahusika na:

Kuchagua njia bora ya usafirishaji baharini, angani, au kwa barabara;

Kuratibu mizigo midogo kwa maana ya loose cargo au mizigo mikubwa kwa maana full container.

Kuhakikisha bima ya usafirishaji imekamilika;

Kutoa ratiba ya safari (shipment schedule) na kufuatilia meli au ndege hadi kufika bandarini.

Kwa maneno mengine, forwarding ni kama project management ya safari ya mzigo wako ΓÇö kuhakikisha kila kitu kipo sawa kabla haujafika kwenye hatua ya forodha.

Clearing Ni Taratibu za Forodha

Baada ya mzigo kufika nchini, unahitaji kupitishwa rasmi na mamlaka husika kama TRA, TBS, TFDA, na TICTS kabla ya kutoka bandarini.
Hii ndiyo inaitwa Clearing.
Kazi kuu za clearing ni:

Kuandaa na kuwasilisha nyaraka muhimu kama Bill of Lading, Invoice, Packing List, na Import Declaration Form (IDF);

Kutoa declaration kwenye mfumo wa TRA;

Kufanya malipo ya kodi na ada;

Kuratibu ukaguzi wa mzigo (inspection) na hatimaye release.

GNM Trading, kama clearing agent, inasimamia mchakato huu wote kwa uwazi, ikihakikisha mteja anaepuka ucheleweshaji, rushwa, au malipo yasiyo rasmi.
Clearing inahusu zaidi mchakato wa kisheria na kiutaratibu wa kuidhinisha mzigo wako kuingia nchini.

Clearing & Forwarding Logistics East Africa Cargo

Comments

1
Leave a Comment
Your email won't be published.
A
azizi
Jun 13, 2026 · 2:18 PM

this is the best

Replying to azizi