Home Blog Article
Business Insights 4 min read

Queenie Masanja kuwa Balozi wa Gnm cargo

M
Meshack21
GNM Cargo Editor
Nov 10, 2025 37 views 0 comments

GNM CARGO tunafuraha kumtangaza na kumkaribisha rasmi Queenie Masanja kuwa Balozi wa Kampuni yetu. Mapokezi yake yamefanyika katika Hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam, ikiwa ni mwanzo wa safari mpya pamoja naye. Tumechagua kufanya kazi na Queen Masanja kwa sababu anaamini kile tunachoamini; Uaminifu, Ubora, na Huduma ya Viwango vya Kimataifa, anajua thamani ya Biashara za Watanzania, lakini pia anataka kuona GNM CARGO ikifika mbali zaidi. Kama GNM CARGO, ahadi yetu kwa wateja na wadau wetu inabaki ile ile; Kutoa huduma bora, za kuaminika, salama na kwa wakati. Karibu Sana Queen Masanja. Pamoja tutaendelea kujenga madaraja ya biashara na kusafirisha ndoto za wengi.

Huduma za Bei Nafuu kwa SMEs

GNM inatoa services za shipping na logistics kwa gharama nafuu, zikiwa:

Consolidation ya mizigo midogo kuokoa gharama za kontena;

Chaguo la shipping kwa bahari au ndege kulingana na bajeti;

Ufuatiliaji wa real-time ili wateja wawe na uwazi wa kila hatua.

Hii inarahisisha SMEs kuagiza mizigo kutoka China au nchi nyingine bila kuvunja bajeti.

Ushauri wa Kibiashara

GNM hutoa ushauri wa kibiashara na logistics planning:

Kuandaa mchakato wa import bila makosa ya kisheria;

Kufahamu taratibu za forodha na mabadiliko ya TRA;

Ushauri wa packaging, labeling, na uhamishaji wa bidhaa ili kupunguza hasara.

Ushauri huu unawawezesha SMEs kufanya maamuzi sahihi na kuongeza ufanisi wa biashara zao.

Urahisi wa Malipo na Ufuatiliaji

Kupitia platform ya kidigitali, wateja wa SMEs wanaweza:

Kufanya malipo kwa urahisi;

Kufuatilia mzigo kwa hatua zote, kutoka bandari hadi dukani;

Kupokea ripoti sahihi za gharama na muda wa usafirishaji.

Hii inawawezesha wafanyabiashara ndogo kupanga vizuri fedha zao na operations, huku wakiwa na uhakika mzigo wao unafika kwa usalama na kwa wakati.

Business Insights Logistics East Africa Cargo

Comments

0
Leave a Comment
Your email won't be published.

No comments yet — be the first to share your thoughts!